Language: English

Ndugu Watanzania nchini Canada na Cuba


Fellow Tanzanians in Canada and CubaYah: USAJILI WA WATANZANIA NCHINI CANADA
Re: REGISTER OF TANZANIANS IN CANADA

Bila shaka wengi wenu mnaelewa kuwa katika miaka ya karibuni Serikali ya Tanzania imeweka mikakati na kuongeza juhudi za kujenga mahusiano na Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kwa lengo kuu la kuwahusisha katika mipango na juhudi za maendeleo nchini kwetu.
As you may well be aware, the Government of Tanzania has in recent years increasingly taken deliberate steps to reach out and engage Tanzanians in the diaspora, with a view to harnessing their goodwill, knowledge and other resources in building and consolidating the development of our motherland.

Ili kufanikisha dhamira hii na malengo yake, ni muhimu kwa serikali yetu na watendaji husika kuwa na taarifa sahihi kuhusu walengwa hao: idadi zao, taaluma zao, mahali walipo, n.k. Kwa msingi huo, Ubalozi huu pia unahitaji kuwa na taarifa hizi kuhusu Watanzania wanaoishi katika eneo letu la uwakilishi (Canada na Cuba), na nachelea kuwajulisha kuwa taarifa zilizopo sasa hazitoshi hata kidogo. Ni jukumu letu pamoja kuondoa dosari hii.
In order to optimize these objectives’ achievement, it is imperative for the government and relevant offices to have as clear and pertinent information as possible regarding the diaspora community: size, composition, location, etc. In that respect and with specific regard to this mission’s area of accreditation (Canada and Cuba), I wish to inform you that the requisite information is not adequately available here at the Tanzania High Commission, and it is our common duty to right this wrong.

Kwa hiyo lengo la barua hii ni kuomba msaada na ushirikiano wenu; msambaze ujumbe huu kwa Watanzania wanaoishi katika maeneo yenu ili watambue umuhimu wa jambo hili na wachukue hatua za kujitambulisha hapa Ubalozini. Tungependa wajitambulishe kwa kujisajili, ama kupitia kwenye tovuti yetu chini. Pamoja na ombi hili, napenda kutaja mambo mawili. Mosi, zoezi hili linahusu watu wote waliozaliwa Tanzania pamoja na familia zao (mke/mme na watoto), alimradi wanajitambulisha kuwa ni Watanzania, hata kama wamepata uraia wa Canada au wa nchi nyingine. Pili,jambo hili si geni. Daima Watanzania walio nje ya nchi hutakiwa kujiandikisha kwenye ofisi ya Ubalozi iliyo karibu na ushauri huo umetamkwa wazi kwenye pasipoti zetu (Uk.47).
I am therefore appealing to each and every one of you, wherever you are in Canada or Cuba, to help in this matter by spreading the message to Tanzanians in your respective areas of residence. Ideally, we would like every Tanzanian to register online as provided on our website below. I also wish to make two points clear. First, this appeal is to all natives of Tanzania and their immediate families, who consider themselves as Tanzanians, even though they may have acquired Canadian or other citizenship. Secondly, this is not a new invention. Our government has always demanded Tanzanians abroad to do this and there is a directive in Tanzania passports (page 47) for all Tanzanians abroad…. “at the earliest opportunity to register their names and addresses at the nearest Mission of Tanzania”.

Natanguliza shukrani tele kwa uelewa na ushirikiano wenu.
I thank you for your time, understanding and anticipated cooperation.

BALOZI